Wanamgambo wa M23 wameteka maeneo ya mashariki mwa nchi toka 2021, na kusababisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao huku wakizua mgogoro wa kibinadamu.
Mkataba wa kusitisha mapigano uliotiwa saini Agosti uliimarisha utulivu hapo awali. Lakini toka Oktoba mwishoni M23 imekuwa katika mapigano jimboni Kivu Kaskazini, kuelekea mji muhimu wa kimkakati wa Pinga.
Jumapili waasi hao walifanya mashambulizi katika eneo la Lubero kuelekea Ziwa Edward, ambalo ni sehemu ya mpaka wa DRC na Uganda, kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya ndani na kijeshi vilivyowasiliana kwa simu na shirika la habari la AFP.
Forum