Raia wa Iran leo Ijumaa wameshiriki uchaguzi wa bunge na baraza kuu la viongozi wa dini huku kukiwa na hofu ya idadi ndogo ya watu ya wapiga kujitokeza na waconsevativu wakitarajiwa kuimarisha uongozi wao.
Kiongozi mkuu Ayatollah Ali Khamenei ambaye alitoa wito kwa watu kujitokeza kwa wingi alikuwa wa kwanza kupiga kura yake katika kituo katikati mwa Tehran, televisheni ya taifa imeripoti.
Uchaguzi huo ni wa kwanza nchini Iran tangu kuenea kwa maandamano yaliyozuka baada ya kifo cha Mahsa Amini aliyekuwa chini ya ulinzi kufuatia kukamatwa kwake kwa tuhuma za kukiuka masharti ya mavazi kwa wanawake nchini humo.
Tangu chaguzi za mwisho, Iran imeathiriwa vibaya sana na vikwazo vya kimataifa ambavyo vimepelekea mzozo wa kiuchumi.
Zaidi ya watu milioni 61 kati ya milioni 85 wanastahili kuwapigia kura wabunge pamoja na viongozi wa dini wa baraza la wataalamu chombo kinachosimamia kumchagua kiongozi mkuu wa Iran.