“Rais Vladimir Putin ameomba radhi kutokana na ajali mbaya iliyotokea katika anga ya Russia na ametoa pia salamu za rambirambi za dhati kwa familia za waathirika na amewatakia waliojeruhiwa kupona haraka,” Kremlin ilisema katika taarifa.
Hayo yakiarifiwa, mashirika kadhaa ya ndege yametangaza kusitisha safari za ndege kuelekea miji ya Russia, baada ya wataalamu kutoka nchi za Magharibi na Marekani kudai kuwa ndege ya Azerbaijan inaweza kuwa imetunguliwa na kombora la Russia.
Moscow imejizuia kutoa maelezo kuhusu ripoti kwamba ndege hiyo ilitunguliwa kwa bahati mbaya na mifumo ya ulinzi wa anga ya Russia.
Russia ilisema, mji mkuu wa Chechenya wa Grozny, ambako ndege hiyo ilitarajiwa kutua, ulikuwa umeshambuliwa siku hiyo na ndege zisizo na rubani za Ukraine.
Ndege hiyo ilianguka siku ya Jumatano karibu na mji wa Kazakhstan wa Aktau, na kuua watu 38 kati ya abiria 67