Pia maandamano hayo yamesababisha vifo vya takriban watu watatu, Inspekta Jenerali wa polisi amesema.
Baadhi ya miji mikubwa, ikiwa ni pamoja na mji mkuu Abuja, na ule wa Kano, ulioko kaskazini mwa nchi, ambapo siku ya Alhamisi ilishuhudia mapambano kati ya polisi na waandamanaji na uporaji, ilionekana kuwa tulivu mapema Ijumaa huku maandamano yakitarajiwa kuendelea.
Wakihamasishwa na maandamano yaliyoongozwa na vijana nchini Kenya, Wanigeria walipanga maandamano, chini ya hashtag '#EndBadGovernanceInNigeria' mtandaoni, wakisema yataendelea kwa siku 10.
Waandamanaji wamekasirishwa na mageuzi ya kiuchumi ya Rais Bola Tinubu ambayo yamesababisha mfumuko mkubwa wa bei, kudhoofisha sarafu na kuwasababishia raia wa kawaida wa Nigeria hali ngumu ya maisha.