Papa Francis awanasihi watu kuacha kujilimbikizia mali

Papa Francis akitoa salamu zake za baraka za Pasaka maarufu kama "Urbi et Orbi" ("kwa jiji la Vatican na dunia") katika uwanja wa St. Peter's Square, Vatican, Aprili 21, 2019.

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis ameongoza ibada ya Pasaka, Jumapili, iliyohudhuriwa na maelfu ya waumini na watalii, kwenye Kanisa la St Peters Basilica, mjini Vatican.

Papa Francis ameeleza ametuma salamu za rambirambi kwa jamaa na marafiki wa wale waliouawa katika mashambulizi hayo.

Kanisa Katoliki limeadhimisha Jumapili ya Pasaka wakieleza masikitiko yao kutokana na mashambulizi ya umwagaji damu yaliyofanyika nchini Sri Lanka.

Papa Francis aliongoza Misa ya wazi katika uwanja wa kanisa la Mtakatifu Petro.

Katika sikukuu hii ya Pasaka Wakristo wanasherehekea ufufuo wa Yesu Kristo. Baadaye Papa Francis atatoa hotuba kwa watu wote duniani.

Mwaka huu kumekuwa na matukio yakusikitisha wakati wa msimu wa Pasaka kwanza ni uharibifu wa Kanisa la Paris la Notre Dame lililoungua moto wiki iliyopita na tukio la mauaji huko nchini Sri Lanka, Jumapili.

Papa Francis katika ujumbe wake kwa ulimwengu Jumamosi aliwatahadharisha wanadamu na kuwahimiza umuhimu wa kuacha vitendo vya kukimbilia utajiri na kujilimbikizia mali ambazo ni vitu vya kupita.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.