Timu ya wanasheria wa Lai iliwasilisha tathmini ya kiesheria baada ya Kamati ya Usalama wa Taifa ya Hong Kong (NSC), inayoongozwa na maafisa wakuu wa Hong Kong na China, kuamua kwamba kuruhusiwa kwa wakili mkuu kutoka Uingereza Timothy Owen kunaweza kuathiri usalama wa taifa na kuishauri mamlaka ya Hong Kong kutompa visa.
Matumizi ya mawakili kutoka nje kunafanywa na wote upande wa mashtaka pamoja na upande wa utetezi imekuwa ikiruhusiwa kwa muda mrefu katika nchi hiyo ambayo ilikuwa koloni la Uingereza kama sehemu ya kanuni zake za utawala wa kisheria.
Kukataliwa kwa changamoto ya kisheria ya Lai kumekuja baada ya bunge la Hong Kong, tarehe 10 Mei , kupitisha mswada unaompa kiongozi wa jiji hilo mamlaka ya hiari ya kuwazuia mawakili wa kigeni kwenye kesi za usalama wa taifa, uamuzi kama huo ulishapitishwa na bunge la taifa la China mwezi Desemba.
Wakati akitupilia mbali pingamizi ya Lai, Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu Jeremy Poon, alisema mahakama za Hong Kong kimsingi hazina mamlaka juu ya Kamati ya Usalama wa Taifa.
Wakili wa Lai, Robert Pang hapo awali alidai kwamba endapo mahakama itashindwa kuingilia kati suala hili wakati Kamati ya Usalama wa Taifa inavuka mipaka ya mamlaka yake, Hong Kong itakuwa "inasema kwaheri kwa sehemu kubwa ya sheria za utawala wetu."