Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi amewafukuza kazi mawaziri sita pamoja na Waziri wa Fedha, katika mabadiliko makubwa.
Hakuna sababu iliyotolewa kufuatia hatua yake ya kuwafukuza kazi mawaziri hao wala kutangaza mipango ya kujaza nafasi zao.
Hii ni mara ya pili kwa rais Nyusi kufanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri katika miezi ya hivi karibuni.
Wengine waliofutwa kazi ni Waziri wa madini na nishati, Waziri wa maji na uvuvi, Waziri wa kazi na nyumba.
Wachambuzi wa siasa nchini Msumbiji wanasema kwamba hawajashutushwa na hatua yar ais Nyusi kuwafuta kazi mawaziri hao.
Mwezi Novemba, Nyusi aliwafuta kazi mawaziri wa ulinzi na wa mambo ya ndani na kujaza nafasi zao.