Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 04:36

Wadukuzi waitishia serikali ya Msumbiji watavujisha siri


Udukuzi wa Mitandao
Udukuzi wa Mitandao

Wadukuzi wa mitandao wamesema wamedukua zaidi ya tovuti 30 nchini Msumbiji, baada ya serikali kutangaza kwamba ilikuwa imezima udukuzi huo.

Kundi linalojiita Yemeni Hackers, limedai kuhusika na udukuzi huo.

Wadukuzi wamesema kwamba wamedukua tovuti za wizara 34 ikiwemo Wizara ya Ulinzi.

Tovuti nyingine ambazo zimedukuliwa ni pamoja na ya usimamizi wa majanga ya kitaifa, idara za maji na taasisi ya taifa ya usafiri na ardhi.

Wadukuzi hao wametishia kutoa taarifa muhimu za serikali iwapo hawatapewa pesa wanazotaka.

Kiongozi wa taasisi inayosimamia mfumo wa kielektroniki nchini Msumbiji Erminio Jasse, amesema kwamba hakuna taarifa za serikali zimeibwa.

XS
SM
MD
LG