Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:54

Msumbiji kupanda zaidi ya miche milioni 100


Watu wakiwa kwenye ufukwe wa Paquitequete nchini Msumbiji
Watu wakiwa kwenye ufukwe wa Paquitequete nchini Msumbiji

Msumbiji ambayo ufukwe wake wa bahari umeathiriwa sana kutokana na kuongezeka kwa maji pamoja na dhoruba za mara kwa mara, Jumanne imetangaza mradi wa kupanda zaidi ya miche milioni 100.

Hatua hiyo imechukuliwa ili kurekebisha hali hiyo. Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, mikoko kwenye ufukwe wa Msumbiji wenye urefu wa kilomita 2,500 imeharibiwa vibaya kutokana na kuongezeka kwa maji ya bahari pamoja na uharibifu kutokana na ukataji kuni pamoja na uchomaji makaa.

Wizara ya bahari na maji ya ndani imesema kwamba inapanga kupanda zaidi ya miti milioni 1000 ndani ya miongo mitatu ijayo kwenye majimbo ya Sofala na Zambezi yenye misitu ya mikoko yenye ukubwa wa hekta 185,000, ambazo ni sawa na miji ya Paris, Manhattan na London ikiwekwa pamoja.

Mradi huo unasemekana kutumia satalaiti katika kutathmini maeneo yanayohitaji upandaji miti ikiwa jihudi ya kudhibiti takriban tani 200,000 za gesi ya kabon kila mwaka, ikiwa sawa na kuondoa magari 50,000 yanayotoa moshi barabarani.

XS
SM
MD
LG