Bola Tinubu wa chama tawala cha APC alitangazwa kuwa mshindi kwa asilimia 37. Lakini wapinzania wake, Atiku Abubakari aliyeshika nafasi ya pili, na Peter Obi nafasi ya tatu, walikataa matokeo hayo na kupeleka mashtaka katika mahakama ya juu ya rufaa ya Nigeria.
Wanataka mahakama inayoshughulika na maswala ya uchaguzi kufuta matokeo ya uchaguzi wa rais. Katika utetezi wake, kwenye mahakama ya malalamiko ya uchaguzi wa rais, tume ya uchaguzi ilieleza maombi yaliyowasilishwa na wagombea wa upinzani kuwa hayana uwezo mkubwa na hayaeleweki kitaaluma.
Awali INEC iliomba radhi kwa kuwepo matatizo ya kiufundi ambayo yalivuruga utaratibu wa kutoa matokeo ya uchaguzi kwa njia ya kielectroniki kutoka kwenye vituo vya uchaguzi.
ilisema kwamba kasoro zozote za matokeo kwenye tovuti yake na matokeo yaliyotolewa ana kwa ana yatafanyiwa uchunguzi na kutatuliwa.
Tume ya uchaguzi ilikosolewa na makundi ya waangalizi wa uchaguzi kwa kuwa na upungufu wa viwango vinavyohitajika.