Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:37

Marekani yafanikiwa kukamata fedha za kifisadi zilizo takatishwa kutoka Nigeria


Diezani Alison-Madueke
Diezani Alison-Madueke

Wazira ya Sheria ya Marekani imesema imefanikiwa kupata  kiasi cha dola milioni 53 fedha taslimu ikiwa ni pamoja na thamani ya mali za mshtakiwa – na hawala yenye thamani ya dola milioni 16.

Kulingana na tangazo lililotolewa na Wizara ya Sheria ya Marekani limesema huu ni uamuzi wa mwisho wa kesi mbili za madai ambao unataka kukamatwa kwa mali mbalimbali za kifahari ambazo zilikuwa zimetokana na kipato cha makosa ya ufisadi nje ya nchi na fedha hizo kutakatishwa ndani na kupitia Marekani.

Kulingana na nyaraka za mahakama, kuanzia mwaka 2011 hadi 2015, wafanyabiashara Kolawole Akanni Aluko na Olajide Omokore walishirikiana na wengine kutoa rushwa kumpa Waziri wa zamani wa Rasilmali za Mafuta, Diezani Alison-Madueke, aliyekuwa anasimamia kampuni ya mafuta inayo milikiwa na serikali ya Nigeria.

Matokeo yake, Alison-Madueke alitumia ushawishi wake kuendesha mikataba yenye faida ya mafuta kwa makampuni yaliyokuwa yanamilikiwa na Aluko na Omokore.

Faida iliyopatikana kutokana na mikataba waliyopewa kinyume cha sheria ilikuwa na thamani ya jumla ya zaidi ya dola milioni 100 ambazo baadae zlitakatishwa ndani ya nchi na kupitia Marekani na zilitumiwa kununua rasilmali mbalimbali kupitia makampuni ya Shell, zikiwemo biashara za majengo ya kifahari huko California na New York na pia boti ya Galactica Star aina ya superyacht yenye urefu wa mita 65.

Biashara ya majumba ilitumika kama rehani ya kupata mikopo iliyotolewa kwa Aluko na makampuni ya Shell aliyokuwa anayadhibiti. Kama sehemu ya mchakato wa kutaifisha mali hizo, vitu vilivyowekwa rehani vilikombolewa.

XS
SM
MD
LG