Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 12:52

Peter Obi wa Nigeria aenda mahakani


Mgombea Urais wa Chama cha Labour nchini Nigeria, Peter Obi, akiwa katika mkutano na waandishi wa habari huko Abuja Machi 2, 2023. Picha na KOLA SULAIMON / AFP.
Mgombea Urais wa Chama cha Labour nchini Nigeria, Peter Obi, akiwa katika mkutano na waandishi wa habari huko Abuja Machi 2, 2023. Picha na KOLA SULAIMON / AFP.

Mgombea urais wa chama cha upinzani cha Labour nchini Nigeria Peter Obi, amewasilisha malalamiko mahakamani akipinga uchaguzi wa rais wenye utata uliofanyika mwezi uliopita, chama hicho kimesema. Akianzisha kile kinachoweza kuwa kampeni ndefu ya kisheria inayoweza kudumu kwa miezi kadhaa.

Kumekuwepo na changamoto nyingi za kisheria kuhusu matokeo ya chaguzi za urais ziliopita nchini Nigeria lakini hakuna aliyefanikiwa.

Katika uchaguzi huo uliofanyika Februari 25, Obi alifanya kampeni kama mtu wa nje, aliyewasisimua vijana na wapiga kura wa mara ya kwanza na kuonekana kuleta ushindani mkubwa, aliwapa matumaini baadhi ya wapiga kura waliotaka mabadiliko baada ya miaka ya mingi ya kupambana na hali ngumu ya maisha na ghasia chini ya utawala wa jenerali wa zamani wa kijeshi na rais anayeondoka madarakani Muhammadu Buhari mwenye umri wa mika 80.

Lakini Obi aliibuka mshindi watatu akiwa nyuma ya mgombea wa chama tawala cha All Progressives Congress (APC) Bola Tinubu ambaye alitangazwa mshindi na mpinzani mkuu kutoka chama cha People's Democratic Party (PDP) Atiku Abubakar, ambao wote walikuwa na nguvu ya kisiasa na uzoefu wa miongo mingi.

“Tunapinga sifa za mgombea ambaye alitangazwa mshindi. Pia tunahoji mchakato ambao ulipelekea kutangazwa mshindi miongoni mwa wagombea wengine” msemaji wa chama cha Labour Yunusa Tanko aliliambia shirika la habari la Reuters.

Mahakama ya Rufaa itakaa kama mahakama na ina siku 180 kusikiliza kesi hiyo na kutoa uamuzi kuhusu changamoto zilizowasilishwa na Obi. Atiku pia amesema atawasilisha malalamiko yake mahakamani, ana mpaka saa sita usiku, siku ya Jumatano kuwasilisha malalamiko.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

XS
SM
MD
LG