Ni Marekani tu inayoweza kushawishi Israeli isishambulie Rafa - Abbas

  • VOA News

Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas

Rais wa Mamlaka ya  Palestina Mahmoud Abbas alisema Jumapili  kwamba ni Marekani pekee inayoweza  kuizuia Israel kushambulia mji wa mpakani wa Rafah katika Ukanda wa Gaza.

Abbas aliongeza kuwa shambulio hilo, ambalo anatarajia litafanyika ndani ya siku chache zijazo, linaweza kuwalazimisha Wapalestina wengi kukimbia eneo hilo.

"Tunatoa wito kwa Marekani kuiomba Israel isiendelee na mashambulizi ya Rafah. Marekani ndiyo nchi pekee inayoweza kuizuia Israel kufanya uhalifu huu," Abbas aliuambia mkutano maalum wa Baraza la Uchumi la Dunia katika mji mkuu wa Saudi Riyadh. .

Israel, ambayo imetishia kwa wiki kadhaa kufanya mashambulizi makubwa kwenye mji huo ikisema lengo lake ni kuangamiza vikosi vya Hamas vilivyosalia huko, ilizidisha mashambulizi ya anga yaliyolenga Rafah wiki iliyopita.

Nchi za Magharibi, ikiwa ni pamoja na mshirika wa karibu wa Israel, Marekani, zimeiomba ijizuie kushambulia mji huo wa kusini, ulio karibu na mpaka wa Misri na unaowahifadhi zaidi ya Wapalestina milioni moja waliokimbia mashambulizi ya miezi saba ya Israel dhidi ya maeneo mengine ya Gaza.