Kabla ya mazungumzo hayo, Rais wa Marekani Joe Biden aliwaandikia viongozi wa Misri na Qatar akiwataka watoe shinikizo kwa Hamas kukubaliana na kutii makubaliano, afisa mkuu wa utawala aliiambia AFP Ijumaa usiku.
Marekani, Qatar na Misri zimeshiriki kwa miezi kadhaa katika mazungumzo ya faragha ili kuwasilisha usitishaji vita na kubadilishana mateka wafungwa wa Kipalestina, lakini hazijachukua hatua yoyote tangu kufikiwa kwa mapatano ya wiki moja mwezi Novemba.
White House ilithibitisha kuwa mazungumzo yatafanyika mwishoni mwa juma hili mjini Cairo, lakini haikuzungumzia taarifa za vyombo vya habari vya Marekani kwamba Mkurugenzi wa CIA Bill Burns atahudhuria, pamoja na mkuu wa kijasusi wa Israel David Barnea, Waziri Mkuu wa Qatar Mohammed bin Abdulrahman Al-Thani na mkuu wa Ujasusi wa Misri Abbas Kamel.
Forum