Juhudi za kidiplomasia ziliongezeka leo Jumapili kufikia makubaliano ya muda mrefu ya kusitisha mapigano na kuachiliwa kwa mateka huko Gaza, wakati Israel ikifanya mashambulizi zaidi ya anga na makombora katika eneo hilo lililoharibiwa na vita.
Video mpya ya mateka wawili wanaoshikiliwa na wanamgambo wa Hamas tangu shambulizi la Oktoba 7 la kundi hilo lilichochea ghadhabu mpya nchini Israel, ambako waandamanaji wamezidisha shinikizo kwa serikali kufikia makubaliano.
Upinzani wa ulimwengu kufuatia mgogoro wa kibinadamu huko Gaza pia umekuwa ukiongezeka, huku viongozi wa dunia na makundi ya misaada wakionya kuwa uvamizi wa Israel katika mji wa kusini wa Rafah utasababisha machafuko maafa makubwa kwa raia.
Rais wa Palestina Mahmud Abbas ameiomba Marekani leo Jumapili kuizuia Israel kuvamia Rafah, ambapo alisema itakuwa “janga kubwa sana katika historia ya watu wa Palestina”.
Forum