Rais Denis Sassou Nguessou wa Jamhuri ya Congo huenda akachukua hatua za kisheria baada ya jina lake kutajwa kwenye nyaraka za siri za 'Pandora Papers’, kulingana na waziri wake wa habari aliyenukuliwa na kituo cha Redio ya Ufaransa, RFI.
Kulingana na nyaraka hizo Rais Sassou Nguesso anamiliki kampuni inayosimamia migodi ya almasi nchini Congo.
Maafisa wa serikali ya Congo wanakanusha jambo hilo na waziri wa habari Thierry Moungalla amelaani kutolewa kwa nyaraka hizo za siri na kusema kwamba rais anaweza kuvishtaki vyombo vya habari vilivyotangaza ripoti hiyo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa ofisi ya mwendesha mashtaka ya Kenya Noordin Haji ameliambia gazeti la Daily Nation la kenya kwamba ofisi yake itawachunguza watu waliotajwa kwenye nyaraka za Pandora na kuona kama zitasaidia kubani ikiwa kuna uhalifu umetendeka kutokana na fedha zilizotajwa.
Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari