Akipatiwa ulinzi mkali na polisi, Salwan Momika, mwenye umri wa miaka 37 aliyekimbilia Sweden miaka kadhaa iliyopita, siku ya Jumatano alikanyaga Qurani kabla ya kuwasha moto kurasa kadhaa nje ya msikiti mkubwa kabisa wa Stockholm.
Polisi wa mji mkuu wa Sweeden walimpatia kibali cha kueleza malalamiko yake chini ya misingi ya uhuru wa kujieleza, lakini baadaye walisema walianza uchunguzi kuhusu uchochezi ulofanywa na mtu huyo.
Tukio hilo la kuichoma Kurani lilitokea wakati waislamu kote duniani walikua wanasherehekea sikukuu ya Eid al-Adha na wakati ibada ya Hija inayofanyika kila mwaka ya Makka nchini Saudi Arabia ikielekea ukingoni.
Rais Recep Tayyip Erdogan alisema leo Alhamnisi ameilaani Sweden kwa kuruhusu kitendo hicho , na kuendeza kwamba jimbo hilo linaongeza wingu kwenye nafasi ya taifa hilo la Ulaya Kaskazini kujiunga na Nato.
Iraq ililaani uamuzi wa maafisa wa usalama wa Sweeden ya kumpa kibali mtu huyo mwenye "msimamo mkali" kuchoma Qurani.
Wizara ya mambo ya nje ya Baghdad imesema "Matukio haya yanachochea hasira miongoni mwa waislamu kote duniani na ni uchochezi wa hatari."
Imam wa dhehebu la ki-Shia mwenye ushawishi mkubwa nchini Iraq, Moqtada Sadr alitoa wito maandamano nje ya ubalozi wa Sweeden ulioko katika mji wa Baghdad, na kutoa shinikizo la kuondolewa kwa balozi huyo, akidai kuwa taifa lake "lina chuki dhidi ya Uislamu".
Misri, ilikiita kitendo hicho cha uchomaji wa Qurani kuwa ni "kitendo cha aibu kinachochochea hasira za Waislamu" walipokuwa wakisherehekea sikukuu ya Eid.
Umoja wa nchi za Kiarabu wenye makao yake mjini Cairo umelitaja tukio hilo kuwa "mashambulizi lililolenga msingi wa imani yetu ya Kiislamu".
Mshauri wa rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu Anwar Gargash aliandika ujumbe wa Teeter kuwa nchi za Magharibi "lazima zitambue kwamba haziwezi kuzilazimisha nchi nyingine za dunia kufuata mfumo wake wa maadili.”
Kuwait ilitoa wito kwa watendaji "vitendo vya chuki" kama hivyo wafikishwe mahakamani na "kuzuiwa kutumia kanuni ya uhuru kama njama ya kuhalalisha chuki dhidi ya Uislamu au imani yoyote takatifu".
Kitendo cha kuchoma Qurani pia klilaaniwa na Baraza la Ushirikiano la nchi za Ghuba lenye wanachama sita ikiwemo Moroko, ambayo imemrudisha balozi wake kutoka Stockholm.
Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP