Nchi sita, ikiwemo Ethiopia, zakubaliwa kujiunga na jumuiya ya BRICS

China-Africa Leaders' Roundtable Dialogue

Jumuiya ya BRICS ya mataifa yanayoendelea kiuchumi ulikubaliana siku ya Alhamisi kuzikaribisha Saudi Arabia, Iran, Ethiopia, Misri, Argentina na Umoja wa Falme za Kiarabu katika hatua inayolenga kuharakisha msukumo wake wa kufanyia mabadiliko utaratibu wa dunia unaouona kuwa umepitwa na wakati.

Jumuiya ya BRICS ya mataifa yanayoendelea kiuchumi ulikubaliana siku ya Alhamisi kuzikaribisha Saudi Arabia, Iran, Ethiopia, Misri, Argentina na Umoja wa Falme za Kiarabu katika hatua inayolenga kuharakisha msukumo wake wa kufanyia mabadiliko utaratibu wa dunia unaouona kuwa umepitwa na wakati.

Katika kuamua kuunga mkono upanuzi, wa kwanza wa jumuiya hiyo katika kipindi cha miaka 13, viongozi wa BRICS waliacha mlango wazi wa upanuzi wa siku zijazo, huku mataifa mengi zaidi yakionyesha nia ya kujiunga na kikundi ambacho wanatumaini kinaweza kusawazisha uwanja wa kimataifa.

Upanuzi huo unaongeza uzito wa kiuchumi kwa BRICS, ambayo wanachama wake kwa sasa ni China, nchi ya pili kwa uchumi mkubwa duniani, pamoja na Brazil, Russia, India na Afrika Kusini.

Unaweza pia kuinua azma yake iliyotangazwa ya kuwa muungano muhimu zaidi kwa upande wa Kusini mwa dunia.

Lakini mvutano wa muda mrefu pia unaweza kuendelea kati ya wanachama ambao wanataka kuimarisha nguzu za jumuiya hiyo, ili kushindana na nchi za Magharibi - haswa China, Russia, na sasa Iran - na wale ambao wanaendelea kukuza uhusiano wa karibu na Marekani na Ulaya.

"Upanuzi huu wa wanachama ni wa kihistoria," Rais wa China Xi Jinping, mtetezi mkuu wa upanuzi wa kundi hilo, alisema.

"Inaonyesha azimio la nchi za BRICS kwa umoja na ushirikiano na nchi nyingi zinazoendelea," aliongeza.

Wanachama hao sita wapya watajiunga rasmi Januari 1, 2024, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alisema alipozitaja nchi hizo wakati wa mkutano wa viongozi wa siku tatu uliofanyika mjini Johannesburg.