Nchi 15 zasaini Mkataba wa Biashara RCEP unaoipa China maslahi makubwa

Viongozi wa nchi 15 za Asia na Pacific walioshiriki latifa Mkutano wa 3 wa ushirikiano mpana wa uchumi wa kikanda (RCEP).

Viongozi wa nchi 15 za Asia na Pacific Jumapili wamesaini mkataba wa ushirikiano mpana wa uchumi wa kikanda (RCEP) pembeni ya mkutano wa mwaka wa Umoja wa Mataifa ya Asia ya Kusini Mashariki, ASEAN, bila ya Marekani kuwepo.

Mkataba huo, uliosainiwa kupitia mawasiliano ya mtandao, unabuni jumuia kubwa zaidi ya kibiashara duniani na itahusisha kiasi cha theluthi moja ya shughuli za kiuchumi duniani.

Waziri Mkuu wa Vietnam Nguyen Xuan Phuc aliongoza mkutano huo amesema kwamba .

“Na ninafuraha kusema kuwa baada ya miaka 8 ya kazi ngumu, hivi leo, tumehitimisha mazungumzo ya RCEP tayari kusiani mkataba.”

Phuc ameongeza kuwa “makubaliano hayo yatasaidia uchumi wa dunia na kikanda kukabiliana na vikwazo na changamoto zinazotokana na COVID-19 na athari za kupungua biashara duniani.”

Waziri Mkuu wa Vietnam Phuc anasema : "Kiongozi huyo alisisitiza kwamba kumalizika kwa mazungumzo ya RCEP, na kupatikana mkataba mkubwa zaidi wa biashara huru duniani, utapeleka ujumbe mzito kuthibitisha jukumu la kuwa mbele kwa nchi za Asia katika kusaidia mifumo ya ushirikiano wa kibiashara, kwa kutengeneza umbile jipya la kibiashara katika kanda, kuwezesha uwepesi ulio endelevu wa biashara, na kuimarisha usambazaji wa bidhaa uliokuwa umeyumbishwa na COVID-19 na kusaidia kufufua uchumi baada ya janga hili.”

Mkataba huu, ambao awali ulipendekezwa mwaka 2012, utapunguza ushuru katika biashara kati ya nchi zilizosaini na kufungua huduma za biashara.

RCEP ina wanachama 10 kutoka nchi za ASEAN ikiwemo China, Japan, Korea Kusini, Australia na New Zealand, lakini Marekani haikushiriki.

Wachambuzi wanaona mkataba huu unatoa maslahi makubwa kwa China katika kueneza ushawishi wake.