Hafla hiyo kwenye kijiji cha Chepkorio ilihudhuriwa na viongozi mashuhuri wakiwemo wanasiasa, wakiongozwa na rais wa Kenya, William Ruto, pamoja na Rais wa Chama cha Riadha ya Duniani Sebastian Coe.
Kiptum mwenye umri wa miaka 24 alikuwa ameshiriki mbio za kimataifa mara tatu, kila moja ikiingia kwenye rekodi ya 7 bora katika historia ya mbio hizo. Oktoba mwaka jana Kiptum alivunja rekodi ya dunia mjini Chicago baada ya kumaliza mbio hizo kwa saa 2 na sekunde 35, akimshinda bingwa mwenzake Eliud Kipchoge kwa sekunde 34.
Mkuu wa raidha wa Kenya Jack Tuwei akitoa hotuba katika mazishi hayo amesema kwamba nyota ya Kiptum ilikuwa inang’aa, na kwamba dalili zote ziliashiria kwamba angevunja rekodi ya kukimbia chini ya muda wa saa mbili.