Mwanamuziki wa Marekani R.Kelly afungwa miaka 30 gerezani

R Kelly akitoka kwenye kituo cha Daley mjini Chicago baada ya kesi yake ya matunzo ya mtoto May 8, 2019. Picha na AP/Matt Marton, File.

Jaji wa mahakama ya Serikali kuu nchini Marekani imempa mwana muziki R. Kelly kifungo cha miaka 20 jela, baada ya kupatikana na hatia ya kutazama ponografia ya watoto na kuwashawishi watoto kufanya ngono.

Lakini amesema mwanamuziki huyo atatumikia vifungo takribani vyote kwa wakati mmoja ikiwemo kifungo cha miaka 30 adhabu iliyotolewa mwaka jana kuhusiana na mashtaka ya kesi ya ulaghai, shirika la habari la Associated Press limeripoti.

Jaji wa Wilaya Harry Leinenweber pia alimuamuru Kelly kutumikia kifungo cha mwaka mmoja gerezani kufuatia adhabu aliyopewa huko New York.

Swali la msingi kuhusiana na hukumu hiyo linaegemea Chicago, mji aliozaliwa Kelly endapo jaji Leinenweber atamuamuru mwamamuziki huyo mwenye umri wa miaka 56 kutumikia vifungo hivyo kwa pamoja au mara baada ya kumaliza hukumu yake ya New York ya mwaka 2021. Kwa pamoja inakuwa sawa na kutumikia kifungo cha maisha .

Hata hivyo pamoja na hukumu ya kifungo cha Alhamisi Kelly hatatumikia zaidi ya miaka 31. Hii inaimanisha kuwa atastahili kuachiwa wakati akiwa na umri kati ya miaka 80, ukimpa matumaini kuwa siku moja atatoka jela akiwa hai.

Chanzo cha Habari hii ni Shirika la habari la Associated Press