Marufuku hiyo pia inamaanisha wafanyikazi wa Tume ya Ulaya hawawezi kutumia programu hiyo ya kubadilishana video, inayomilikiwa na China kwenye vifaa vya kibinafsi, ikiwa ni pamoja na simu ambazo zimewekwa programu rasmi, msemaji huyo alieleza, akithibitisha ripoti ya tovuti ya habari ya Euractiv.
"Ni lazima wafanyikazi waondoe programu hiyo haraka iwezekanavyo, na wanapaswa kufanya hivyo kufikia tarehe 15 Machi," tume hiyo ilisema.
TikTok, ambayo kampuni mama yake ya ByteDance ni ya Kichina, na imekabiliwa na uchunguzi unaoongezeka, unaofanywa na nchi magharibi katika miezi ya hivi karibuni, kutokana na hofu kuhusu ni kiasi cha data ya watumiaji, ambacho huenda kikafikia serikali ya China.
Marekani mwaka jana ilipiga marufuku programu hiyo kutoka kwa vifaa vya serikali kuu, na baadhi ya wabunge wa Marekani wanajaribu kupiga marufuku TikTok kwendelea kutumika nchini Marekani.
Mwezi uliopita, iliripotiwa kuwa serikali ya Uholanzi iliwashauri maafisa wa umma kujiepusha na programu hiyo kutokana na wasiwasi kama huo. Mnamo Novemba, TikTok ilikubali baadhi ya wafanyikazi nchini China wanaweza kufikia data ya watumiaji wa Ulaya.