Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:33

Facebook kufuta kazi idadi kubwa ya wafanyakazi - Vyanzo vya habari


Mark Zuckerberg, Mkurugenzi Mtendaji wa Facebook
Mark Zuckerberg, Mkurugenzi Mtendaji wa Facebook

Kampuni ya Meta, inayomiliki mtandao wa Facebook, inajiandaa kuanza kuwaachisha kazi idadi kubwa ya wafanyakazi wake wiki hii, kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya Marekani.

Mpango huo, ambao uliripotiwa kwa mara ya kwanza na gazeti la The Wall Street Journal, unatarajiwa kuathiri maelfu ya wafanyakazi na itakuwa mara ya kwanza kwa kampuni hiyo kupunguza wafanyakazi kwa kiwango hicho katika historia yake ya miaka 18.

Hatua hiyo inatarajiwa kuchukuliwa mapema Jumatano, kwa mujibu wa walionukuliwa na gazeti hilo.

Kuachishwa kazi kutafuatia msururu wa kupunguzwa kwa wafanyakazi katika kampuni za teknolojia katika miezi ya hivi karibuni, zikiwemo Twitter, Microsoft, Lyft na Stripe.

Meta, pamoja na makampuni mengine ya teknolojia, yanakabiliwa na shinikizo za kiuchumi katika nyanja kadhaa, ikiwa ni pamoja na kupunguza kasi ya ukuaji wa uchumi, kupanda kwa viwango vya riba ambavyo vinawalazimu watangazaji wa kidijitali kupunguza, na kuongeza viwango vya riba, ambayo inafanya kuwa ghali zaidi kwa kampuni kama Meta kukopa pesa.

Kampuni za mitandao ya kijamii pia zinakabiliwa na ushindani unaokua kutoka kwa wapinzani wapya kama TikTok na Snapchat.

Twitter ilipunguza karibu nusu ya wafanyikazi wake wiki iliyopita baada ya bilionea Elon Musk kununua kampuni hiyo.

XS
SM
MD
LG