Mito katika jimbo la pwani la magharibi la Gujarat imevunja kingo zake na zaidi ya watu 23,000 wamehamishwa kutoka kwenye nyumba zao, kulingana na ripoti.
Gazeti la Business Standard lilisema watu 15 wamefariki tangu Jumatatu katika wilaya nane za jimbo hilo.
Wavuvi wameshauriwa kutokwenda baharini huku waziri kiongozi Bhupendra Patel akitoa tahadhari kwenye mtandao wa kijamii kwa wavuvi.
Mvua za masika husababisha uharibifu mkubwa kila mwaka, lakini wataalam wanasema mabadiliko ya hali ya hewa yanabadilisha mwenendo wa hali ya hewa na kuongeza idadi ya matukio mabaya ya hali ya hewa.
Jimbo la kaskazini mashariki la Tripura lilikumbwa na mafuriko na maporomoko ya ardhi wiki iliyopita, na zaidi ya watu 20 walipotea maksha.
Katika nchi Jirani ya Bangladesh mto Imefuriko na kusababisha muva zimesababisha mafuriko makubwa na vifo vya watu wasiopungua 40 katika kipindi hicho huku wakaazi karibu 300,000 wakitafuta katika makazi ya dharura.