Kevin Kangethe alikuwa amezuiliwa wakati akisubiri kurejeshwa Marekani kuhusiana na kifo cha Margaret Mbitu mwishoni mwa mwaka jana, lakini alitoroka kwenye kituo cha polisi Jumatano jioni.
“Hii inatia aibu” mkuu wa polisi Nairobi Adamson Bungei alisema
“Tumewakamata maafisa wanne waliokuwa zamu wakati Kangethe alipotoroka kueleza kilichotokea na tunamtafuta” aliwaambia waandishi wa habari.
Polisi wa Marekani na Kenya wameanzisha msako baada ya Mbito kugundulika amechomwa kisu na kufa ndani ya gari ilyoikuwa imeegeshwa katika uwanja wa ndege wa Logan uliopo Boston mwezi Novemba.
Amri ya kukamatwa kwa Kangethe ilitolewa baada ya kutoroka Marekani kwenda Kenya alikozaliwa, ambako alikamatwa mwishoni mwa mwezi januari.
Polisi imesema mshukiwa, ambaye taarifa mbalimbali za vyombo vya habari zimeripoti zikisema Kangethe alikuwa na umri wa kati ya maika 40 au 41, alikuwa ameondolewa kutoka mahabusu siku ya Jumatano kwa ajili ya kukutana na mwanasheria wake ambaye pia amekamatwa.
Vyomvo vya habari vimeripoti kuwa alikuwa amedandia matatu, mabasi madogo binafsi yanayotumiwa sana kwa usafiri na Wakenya .
Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP