Barabara za mji mkuu wa Guinea wa Conakry Jumatatu zimebaki tupu, na biashara kufungwa, kufuatia mgomo wa kitaifa wa wafanyakazi wakiwemo wachimba madini ,wakiitisha nyongeza za mishahara miongoni mwa mengine.
Tiafa hilo la Afrika Magharibi linaongozwa na kundi la kijeshi lililofanya mapinduzi 2021, na limekuwa likizima maandamano ya mara kwa mara dhidi ya serikali.
Chama cha wafanyakazi cha Guinea wiki iliopita kilitangaza mgomo wa kitaifa, bila kusema utakapomalizika, ukijumuisha sekta za umma na za kibinafsi.
Miongoni mwa masuala yanaoitishwa ni pamoja na kuachiliwa kwa Katibu Mkuu wa Muungano wa wanahabari wa Guinea, ambaye amefungwa jela, kushuka kwa bei za vyakula, kuondolewa kwa masharti ya internet, pamoja na kutimizwa kwa ahadi za nyongeza ya mishahara iliyofikiwa Novemba.