Mlipuko huo uliharibu matanki ya mafuta na kuwalazimisha mamia ya watu kukimbia nyumba zao zilizoharibiwa.
Watu 14 waliuwawa na wengi 190 kujeruhiwa katika mlipuko huo kwenye taifa la Afrika magharibi kwenye kituo kikuu cha mafuta, ambao ulipiga wilaya ya Kaloum katikati mwa Conakry jumatatu asubuhi.
Katika maelezo yake ya awali kuhusu uharibifu uliotokea serikali ilisema matanki 13 ya mafuta yalikuwa hayafanyi kazi wakati mengine matano hayakuathiriwa.
Viwanda vingi vya nishati nchini guinea hasa hasa vile vinavyosambaza umeme katika mji mkuu vinatumia mafuta ya Diesel
Mapema wafanyakazi wa zimamoto walipambana kudhibiti moto huku kukiwa na moshi ukionekana maili kadhaa kutoka katika eneo la mlipuko. Nchi jirani ikiwemo Senegal zilituma wafanyakazi wa dharura kusaidia juhudi za uokozi.
Forum