Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa linasema hatua hiyo imewaacha bila ya maamuzi mengine isipokuwa kuwasaidia wale ambao wako katika mazingira hatarishi zaidi.
Katika kambi ya wakimbizi ya Palorinya nchini Uganda, bustani zimejaa mahindi – lakini mavuno yatakuwa machache.
Baba wa watoto tisa Idd Alfred anasema katika siku zilizopita, shamba lake liliweza kumpatia magunia mawili ya mahindi.
Lakini kutokana na ukame wa muda mrefu mwaka huu, hatarajii chochote.
“Unapoangalia mazao haya, hayastahmili ukame. Yanahitaji mvua za mara kwa mara ili kupata mavuno mazuri. Bila ya mvua, sipati chochote; yatakufa kabisa,” anasema Alfred.
Uganda ni Makazi ya Wakimbizi Milioni Moja
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi linasema Uganda ni makazi ya wakimbizi milioni moja na nusu na waomba hifadhi, na kuifanya kuwa nchi ya Afrika yenye idadi kubwa ya wakimbizi.
Serikali ya Uganda inatoa kwa kila familia ardhi ya ukubwa wa futi tisa kwa tisa kwa ajili ya nyumba na shamba dogo.
Lakini haitoshi kuzisaidia familia za wakimbizi kama mama wa watoto watano, Naima Pony, ambaye anakwenda kwenye mpaka na Sudan Kusini kununua chakula.
Naima Pony anasema “Chakula ni kidogo sana. Watoto wangu wanakua, wanakula sana, ingawaje hakuna chakula. Chakula hakitoshi.”
UN imepokea asilimia 27 tu ya ufadhili
Umoja wa Mataifa unasema umepokea asilimia 27 tu ya ufadhili unaohitajika kwa ajili ya wakimbizi nchini Uganda, kwahiyo wamelazimisha kubadili mpango - - kwa mara ya kwanza – lengo la msaada limewekwa kuanza July mosi.
Kaya zinazofikiria kuwa ni zile ambazo ziko katika mazingira hatarishi, kama zile ambazo zinasimamiwa na wanawake au wagonjwa sugu, zitapatiwa asilimia 60 ya mgao wa chakula ambao umependekezwa utolewe kwa mwezi.
Wakimbizi wengine watapatiwa asilimia 30 tu.
Naibu Mkuruenzi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani kwa Uganda, Marcus Prior, anasema maafisa watafuatilia kwa karibu sana, matokeo mabayo kutokana na makato ya chakula. “Tutaangalia masuala kama vile matumizi ya watu katika chakula. Tutaangalia viwango vya lishe. Tutaangalia aina ya mikakati ya kujinusuri ambayo wakimbizi wataitumia kama wako katika shida. Hii itaturuhusu sisi kuichukua kesi yetu kwa wale ambao wanaliunga mkono Shirika la Mpango wa Chakula na majibu ya mkimbizi kwa upana zaidi.”
Kiongozi wa wakimbizi Kenye Moses anasema tayari wanaona matokeo ya ukame na kupunguzwa kwa chakula – baadhi ya wakimbizi wanaoondoka.
“Kaya zetu nyingi hivi sasa zimeachwa katika mikono ya watoto wadogo. Watu wetuwengi wamekwenda zao Sudan Kusini, wakifahamu vyema hali ilivyo huko si nzuri. Watoto hawa wako peke yao, hawawezi kuongoza familia,” Kenyi amefafanua zaidi.
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani linasema linahitaji kiasi cha asilimia 63 ya msaada wa wakimbizi mpaka mwisho wa mwaka huu.