Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 08:17

Sababu zinazopelekea watu wengi kujiua katika kambi ya wakimbizi ya Palorinya nchini Uganda zatajwa


Mkimbizi kutoka Sudan Kusini akipeleka chakula alichopokea kutoka kwa Shirika la Chakula Duniani (WFP) kuingiza katika kambi ya Palorinya kwa ajili ya kuwagawia wengine, iliyoko wilaya ya Moyo kaskazini mwa Uganda, Oct. 26, 2017.
Mkimbizi kutoka Sudan Kusini akipeleka chakula alichopokea kutoka kwa Shirika la Chakula Duniani (WFP) kuingiza katika kambi ya Palorinya kwa ajili ya kuwagawia wengine, iliyoko wilaya ya Moyo kaskazini mwa Uganda, Oct. 26, 2017.

Kambi ya wakimbizi ya Palorinya nchini Uganda inaripotiwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaojiua na majaribio ya kujiuua yanayofanywa na wale wanaoishi katika kambi hiyo.

Mashirika na watu binafsi ambao wanafanya kazi na wakimbizi wanasema kunyimwa chakula na kushindwa kukidhi mahitaji ya msingi ndiyo chanzo kikuu cha hali hiyo.

Tangu kuanza kwa mwaka 2023, Lutheran World Federation, shirika lisilo la kiserikali limekuwa likifanyaka kazi na wakimbizi katika makazi ya Palorinya katika wilaya ya Obongi nchini Uganda, ambako kuna rekodi ya mtu mmoja kujiua na majaribio 20 ya kutaka kujiua.

James Wubam mwenye umri wa miaka 18 amefika Palorinya na mjomba wake. Anasema mke wa mjomba wake huenda kwa makusudi alikuwa akimnyima chakula. Pia alisema ili vigumu sana kwake kumuomba mjomba wake ampe mahitaji ya msingi, ikiwemo mahitaji ya shule. Hana ndugu wa kushirikiana naye masuala haya, na hii ilimuweka katika hali mbaya sana ya msongo wa mawazo.

James Wubam ambaye anatokea Sudan Kusini anasema “nilifikiria kujinyonga. Nilikwenda kwenye baa ya karibu na majirani zangu na kunywa pombe. Nilipofika nyumbani, nilifikiria kujiua.”

Kwa mujibu wa Lutheran World Federation, kati ya Januari na Septemba 2019, Palorinya imerekodi visa vingi vya kujiua katika kambi zote za wakimbizi nchini Uganda, huku kukiwa na majaribio 29 ya kutaka kujiua na 13 yalifanyika. Mwaka 2022, shirikisho hilo linasema, tukio moja la kujiua na 45 yalikuwa majaribio ambayo yaliripotiwa kutokea kwenye kambi.

Isaac Oturi, mwanasaikolojia wa Lutheran World Federation, anasema majaribio takriban 20 ya kujiua hadi hivi sasa mwaka huu yalihusisha vijana wadogo na kuchochewa na mahitaji ambayo hayakutimizwa.

Oturi anasema katika makazi hayo, watu, mikono yao imefungwa. Wanajikimu kwa misaada wanayopewa. “Huwezi kujikimu mwenyewe. Na lililo baya zaidi ni kwamba hata wale walio katika nafasi ya kufanya kazi, kuna fursa chache au hata hazipo za kujikimu kimaisha ambazo zingeweza kusaidia kufanya hali ya maisha kuwa nzuri.”

Zaidi wakimbizi milioni 1.5 nchini Uganda, wengi wao kutokea Sudan Kusini, wako Palorinya ambayo ni mwenyeji wa wakimbizi 123,000. Mwezi Julai, Shirika la Mpango wa Chakula lilianza kulenga misaada ya chakula na fedha taslimu kwa wakimbizi wenye shida. Wakihofia kuwa wataachwa wajihudumie wenyewe, baadhi ya wakimbizi walifikiria kujiua.

Wakimbizi wa Sudan Kusini wakikimbia manyanyaso. Mkimbizi huyu na mtoto wake wako katika kambi ya Palorinya, Uganda. (AP Photo/Justin Lynch)
Wakimbizi wa Sudan Kusini wakikimbia manyanyaso. Mkimbizi huyu na mtoto wake wako katika kambi ya Palorinya, Uganda. (AP Photo/Justin Lynch)

Michael Gaale, mkimbizi kutoka Sudan Kusini anasema aliona jina lake limeorodheshwa chini ya wale ambao familia zao hazipewi chakula, haraka alifikiria jinsi ya kujiondoa huko.

“Watakuita baba wanapotaka kula. Lakini hakuna chakula, hakuna chochote. Siwezi kwenda kufanya kazi kwa watu. Nakaa sehemu moja tu. Ni mbaya sana, bora nijiue,” anasema Gaale.

Kuhakikisha kila kesi inashughulikiwa kwa wakati, mashirika yamewekwa washauri nasaha, ambao pia wanajulikana kama ‘gatekeepers.’ Mshauri Deanga Betty Kenyi anasema inawalazimu kutegemea watu wa kati ili kuwapata wale ambao walijaribu kujiua.

Kenyi anasema “jirani atakuja kwenye na kutoa habari hizo. Halafu tutakwenda kutathmini hali ya mteja ilivyo.”

Huku kukiwa na ufadhili na mwanasaikolojia katika kambi hiyo, waathirika wengi hawapati msaada wanaohitaji.

Forum

XS
SM
MD
LG