Miili kumi zaidi yapatikana Shakahola ambapo wafuasi zaidi ya 200 wa dhehebu 'potofu' walifariki

FILE - Baadhi ya Miili ya waathirika wa dhehebu linasosadikiwa kuwa potofu yapatikana huko katika msitu wa Shakahola nje ya mji wa Malindi, mwambao wa Kenya, Aprili 25, 2023.

Maafisa wa usalama nchini Kenya wamesema miili kumi zaidi imepatikana katika msitu wa shakahola ambako waathirika zaidi ya 200 wadhehebu linalosadikiwa kuwa na imani potofu tayari imepatikana.

Mkuu wa mkoa wa pwani amesema licha ya wale waliokutwa wamekufa jana baadhi ya watu waliokolewa.

Rhoda Onyancha, Mkuu wa Mkoa wa Pwani: Timu ya msako na uokozi imfanikiwa kuwaokoa wanaume watatu. Wanaume watatu watu wa zima, kwa bahati mbaya wakiwa katika hali mahututi na wamepelekwa katika hospitali ya malindi kwa ajili ya matibabu.

Mkuu wa Mkoa aliongeza kuwa: "Tumeshawakamata watu wanne, wote wanaume na wako chini ya ulinzi, wakilisaidia jopo linalofanya uchunguzi.”

Onyancha amesema mamia ya watu bado wanaripotiwa hawajulikani walipo na mamlaka zinaendelea kutafuta mabaki na walionusurika kote katika msitu hiyo kusinimagharibi mwa Kenya.