Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 03:10

Miili mingine 29 yafukuliwa katika msitu wa Shakahola


Aliyejiita kasisi na mwanzilishi wa kanisa la Good News, Paul Nthenge Mackenzie (katikati) alipofikishwa katika mahakama ya Shanzu mjini Mombasa, tarehe 5 Mei 2023.Picha na SIMON MAINA / AFP
Aliyejiita kasisi na mwanzilishi wa kanisa la Good News, Paul Nthenge Mackenzie (katikati) alipofikishwa katika mahakama ya Shanzu mjini Mombasa, tarehe 5 Mei 2023.Picha na SIMON MAINA / AFP

Wachunguzi nchini Kenya wamefukua miili mingine 29 siku ya Ijumaa na kufanya idadi ya waathirika wanaohusishwa na ibada ya kutokula wakiamini siku ya kiama imekaribia kufikia 179, ambapo wengi wao ni watoto.

Polisi wanaamini kwamba miili mingi iliyopatikana katika msitu karibu na mji wa pwani wa Malindi, ulioko Bahari ya Hindi ambao ni wafuasi wa Paul Nthenge Mackenzie, dereva wa teksi ambaye amegeuka kuwa mhubiri anayetuhumiwa kuwachochea wafuasi wake wakae na njaa wafe "ili wakutane na Yesu."

Mvua kubwa imekuwa imetatiza msako na operesheni ya kuchimba makaburi wiki iliyopita wakati zoezi hilo litarejea Jumanne.

Watu wapatao 25 pamoja na Mackenzie wako chini ya ulinzi wa polisi -- na "genge la watekelezaji" waliopewa jukumu la kuhakikisha kuwa hakuna mtu aliyeacha kufunga au kuondoka mafichoni ndani ya msitu huo akiwa hai, alisema Onyancha.

Mackenzie bado hajatakiwa kujibu mashitaka, lakini mahakama iliamuru Jumatano azuiliwe kwa wiki tatu nyingine wakisubiri uchunguzi zaidi kuhusu kile kinachoitwa "Mauaji ya Msitu wa Shakahola".

Mwanzilishi huo wa Kanisa la Good News International mwenye umri wa miaka 50 alijisalimisha tarehe 14 Aprili, baada ya polisi kwanza kudokezwa na kuingia katika msitu wa Shakahola.

Ingawa njaa inaonekana kuwa sababu kubwa ya vifo hivyo, baadhi ya waathirika -- wakiwemo na watoto - walinyongwa, kupigwa au kuzibwa hewa, kulingana na daktari mkuu wa serikali Johansen Oduor.

Nyaraka zilizowasilishwa mahakamani siku ya Jumatatu zilisema baadhi ya maiti zilikuwa zimeondolewa viungo vyao, huku polisi wakidai washukiwa walikuwa wakihusishwa kwa lazima katika uvunaji wa viungo vyao.

Lakini Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki amesihi kuwepo na tahadhari, akiwaambia waandishi wa habari siku ya Jumanne kwamba "hiyo ni nadharia tunayochunguza."
Mchungaji mwingine anayetuhumiwa kuhusishwa na Mackenzie pamoja na miili iliyopatikana msituni aliachiliwa kwa dhamana mahakama ilipokutana wiki iliyopita.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la AFP.

XS
SM
MD
LG