Nemtsov aliyekuwa mkosoaji mkubwa wa rais Vladimir Putin, na pia naibu waziri mkuu wakati wa utawala wa rais Boris Yeltsin, alipigwa risasi na kuuwawa 2015 wakati akivuka daraja moja karibu na Kremlin, mjini Moscow. Mahakama ya Russia 2017 ilitoa hukumu dhidi ya wanaume watano kutokana na mauaji hayo, wakipewa vifungo vya kati ya miaka 11 hadi 20 jela.
Miongoni mwao ni Tamerian Eskerkhanov, ambaye alihukumiwa kama mshirika, na kupewa kifungo cha miaka 14 jela. Machi mwaka huu anesemekana kutia saini mkataba na wizara ya Ulinzi ili kuachiliwa na kujiunga kwenye jeshi.
Maelfu ya wafungwa wa Russia wamejitolea kujiunga kwenye jeshi linalopigana na Ukraine, wakitegemea kuwa huru iwapo watanusurika kwenye uwanja wa vita, kwa mujibu wa msamaha uliotolewa na serikali.