Akizungumza kwenye White House pamoja na Rais Biden, mfalme Abullah alitoa wito wa sitisho la mapigano la mara moja kati ya Israel na Hamas.
“Tunahitaji sitisho la mapigano la kudumu sasa,” alisema, akiongeza kuwa mashambulizi ya ardhini ya Israel kwenye mji wa kusini mwa Gaza wa Rafah wenye msongamano wa watu, yatasababisha kwa hakika janga jingine la kibinadamu.”
Mkutano huo umejiri huku Biden akiendelea kuishinikiza Israel isifanye mashambulizi ya ardhini katika mji huo wa Rafah bila mpango wa kulinda raia wa Palestina ambao wamejazana huko.
Mfalme Abdullah alitarajiwa kumuomba Biden kuunga mkono sitisho la mapigano la mara moja.
Utawala wa Biden umekuwa ukijaribu kufanya mazungumzo ya kufikia sitisho la mapigano ili mateka wanaoshikiliwa na Hamas tangu shambulizi la wanamgambo hao la Oktoba 7 waachiliwe huru.