Melania atembelea kumbukumbu ya kituo cha utumwa Ghana

Mke wa Rais Melania Trump akitembelea nyumba ya makumbusho Ghana Octoba 3, 2018.

Mke wa Rais Melania Trump ametembelea kumbukumbu ya kituo cha zamani cha utumwa Jumatano katika pwani ya Ghana, wakati wa safari yake ya kwanza ya ziara ya wiki moja Afrika.

Trump ametembelea eneo la Cape Coast Castle, jengo lenye karne 17 ambalo hapo awali lilijengwa na Waswidi ikiwa kwa ajili ya biashara ya mbao na dhahabu.

Lakini baadae ikawa kituo kikuu nje ya mji kilicho tumika kusafirisha watumwa kupitia bahari ya Atlantic, ambako watumwa walikuwa wakishikiliwa mpaka pale ilipokuwa tayari kuwasafirisha nje ya nchi “katika safari iliyokuwa inatisha na isiyo julikana hatma yake.”

Shirika la habari la Associate Press linaripoti kuwa mke wa Trump ameeleza kile alicho kiona kuwa “ ni chenye kuibua hisia nzito na amesema kituo hicho “ni kitu ambacho watu wanatakiwa kukitembelea na kujifunza juu ya historia hiyo.”

Wakati wa ziara yake, alikutana pia na wanajamii wa kabila la Fante.

Mke wa rais anatumia ziara yake hiyo nchini Ghana, Malawi, Kenya na Misri kuendeleza kampeni ya “Be Best” aliyo ibuni ambayo ina angaza juu ya ustawi wa watoto kwa ujumla.