Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:01

Melania kuangalia mahitaji ya watoto, wazazi Afrika


Melania Trump
Melania Trump

Mke wa Rais wa Marekani Melania Trump atasafiri Jumatatu kuelekea Afrika, katika ziara yake kubwa ya kwanza akiwa peke yake tangia mumewe achaguliwe kuwa rais.

White House imesema kuwa ziara yake ya siku tano itamchukuwa katika nchi nne –Kenya Ghana, Malawi, na Misri – na “itaangaza juu ya suala la huduma kwa wazazi na watoto wanao zaliwa katika hospitali, elimu kwa watoto, na utamaduni na historia inayo fungamana na kila nchi ya Kiafrika, na namna Marekani inavyoweza kusaidia kila nchi katika safari yake ya kujitegemea.

Maisha bora kwa watoto imekuwa ni angalizo la kampeni ya Trump “Be Best” iliyo zinduliwa mapema mwaka 2018.

Safari yake inaweza ikawa na ugumu fulani kutokana na vitendo na maneno ya mumewe ambaye aliwahi kutumia lugha mbaya kwa kuielezea Afrika.

Judd Devermont, mkurugenzi wa programu ya Afrika katika Kituo cha Mikakati na Tafiti za Kimataifa, amesema, Trump “anayo kazi ngumu ya kufanya wakati wa ziara yake na siyo haki kwa sababu safari kama hiyo siyo jukumu la mke wa rais.

Hata hivyo, Joshua Meservey, mchambuzi wa ngazi ya juu wa sera za Afrika katika taasisi ya Heritage Foundation, anaamini kuwa mwenendo wa Rais Trump hauwezi kuathiri ziara ya Mke wake barani Afrika.

“Nafikiri mahusiano kati ya Marekani na Afrika ni makubwa zaidi kuliko maoni ya rais, na ni kitu kimekuwepo kwa miongo na miongo.” Meservey ameongeza, “Ukweli, ninadhani walio wengi kati ya Waafrika wa kawaida hawakusikia chochote kuhusu hizo kauli za Rais. Zaidi ni watu wasomi ambao wanajishughulisha na matamko ya kisiasa.”

Trump anafuata nyao za wake wa marais wa Marekani walio tembelea bara hilo la Afrika. Hillary Clinton, Laura Bush na Michelle Obama walifanya ziara mara kadhaa katika bara hilo.

XS
SM
MD
LG