Nyota huyo wa filamu amefariki akiwa na umri wa miaka 67, alipata umaarufu kwa picha aliyocheza utotoni ya “Mera Naam Joker,” (My Name is Joker) ilipelekea kukonga nyoyo za mamilioni ya washabiki ikisimulia mapenzi ya utotoni, “Bobby” mwaka 1973.
Habari za kifo chake ilikuwa ni pigo la pili kwa kampuni ya filamu ya Bollywood Hindi na mamilioni ya washabiki wake – baada ya Kapoor kufariki siku moja baadae, msiba huo ukitanguliwa na mcheza filamu mashuhuri Irrfan Khan, aliyefariki kutokana na saratani.
Kapoor aliwahi kutibiwa katika hospitali ya New York kwa mwaka mmoja kabla ya kurejea India mwezi Septemba mwaka 2019. Alikuwa amelazwa katika hospitali ya Mumbai Jumatano.
“Madaktari na wauguzi katika hospitali hiyo wamesema alikuwa akiwaburudisha hadi mwisho wa uhai wake. Alikuwa ni mcheshi na mwenye matuamini ya kuishi kwa kipindi chote cha miaka miwili ya matibabu yake katika mabara mawili alikokuwa akitibiwa,” familia ya Kapoor imesema katika tamko lake.
Kapoor alikuwa ni wa kizazi cha tatu katika familia maarufu ya Bollywood ambayo inamchango mkubwa katika sekta hiyo ya filamu.