Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:09

Prince Harry amchumbia mcheza filamu wa Marekani


Harry na mchumba wake Meghan
Harry na mchumba wake Meghan

Prince Harry wa Uingereza amemchumbia mcheza filamu maarufu wa Marekani Meghan Markle.

Baba yake Harry, Prince Charles, alitangaza hilo katika tamko lake siku ya Jumatatu.

“Prince Charles anafuraha kubwa kutangaza uchumba wa mtoto wake Harry na msanii Meghan Markle.”

Tamko hilo pia limesema kuwa ndoa yao itafanyika kipindi cha kuanza kwa joto 2018 na kuwa “maelezo zaidi kuhusu siku ya ndoa kufungwa yatatangazwa siku za usoni.”

Wapenzi hao wawili walifanya sherehe ya uchumba wao mapema mwezi huu, kwa mujibu wa tamko hilo.

Harry alimfahamisha Malikia na wanandugu wa familia yake, tangazo hilo lilieleza, na "... pia mahusiano yao yalipata baraka zote za wazazi wa Markle."

Tangazo rasmi lilikuwa limetarajiwa baada ya Markle kusema hivi karibuni katika mahojiano yake huko Vanity Fair juu ya mahusiano yake kimapenzi na Prince Harry: Sisi tuko pamoja. Tunapendana.”

Wazazi wa Markle pia wametoa tamko, wakisema “ Tunafuraha isiyo kifani kwa kuwepo mahusiano kati ya Meghan na Harry.

Binti yetu siku zote amekuwa mtu mkarimu na mwenye mapenzi. Kuona mafungamano yake na Harry ambaye pia anasifa kama zake ni sababu ya furaha kubwa kwetu sisi kama wazazi.”

Wazazi wa Markle Thomas Markle na Doris Ragland waliachana.

Markle amepata umaarufu mkubwa katika kazi zake za kuigiza kwenye televisheni.

Msanii huyu ni balozi wa hisani wa shirika la World Vision la Canada, ambalo hufanya kampeni kwa kuhamasisha elimu bora, chakula na afya kwa watoto ulimwenguni.

Pamoja na kazi yake ya misaada ya kibinadamu, pia anajulikana kwa kufanya kampeni juu ya haki za jinsia.

Aliwahi kuolewa kwa kipindi kifupi mwaka 2011 na mzalishaji filamu Trevor Engelson, lakini wakaachana baada ya miaka miwili.

Harry na mchumba wake walionekana mara ya kwanza hadharani mwezi Septemba katika eneo la Invictus Games huko Toronto, ambapo michezo ya wanajeshi walioumia vitani hufanyika.

Mwaka jana, Prince Harry ambaye ni watano katika urithi wa ufalme alitoa tamko akilalamika jinsi vyombo vya habari vilivyo ripoti habari za rafiki yake, akilaani waziwazi “ubaguzi wa rangi na jinsia unaofanywa na mitandao ya jamii na baadhi ya kauli za kigauzi zinazowanyanyapaa watu wa rangi.

Markle ni mwenye asili mbili baba yake ni mzungu na mama yake ni mwafrika.

XS
SM
MD
LG