Mawaziri wa mambo ya nje wa Sudan na Iran wakutana

Waziri wa mambo ya nje wa Sudan, Ali al-Sadiq akiwa Khartoum Februari 9, 2023. Picha na Kitini / WIZARA YA NJE YA URUSI/AFP.

Waziri wa mambo ya nje wa Iran Hossein Amirabdollahian amekutana na waziri wa mambo ya nje wa Sudan Ali al-Sadiq kwa mara ya kwanza tangu uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili kuvunjika miaka saba iliyopita, shirika rasmi la habari la Iran, IRNA liliripoti Alhamisi.

"Kando ya mkutano wa nchi zisizo katika harakati za kutofungamana na upande wowote, ujumbe wetu umekutana na waziri wa mambo ya nje wa Sudan na kujadili jinsi ya kurejesha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Khartoum na Tehran," Amirabdollahian aliandika kwenye ukurasa wake wa tweeter.

"Katika mkutano huu, mazungumzo yaliegemea katika kusuluhisha hali ya kutoelewana kati ya nchi hizi mbili pamoja na kuimarisha uhusiano wa kisiasa na kiuchumi kati ya Tehran na Khartoum," IRNA iliripoti kuhusiana na mkutano huo uliofanyika Baku, mji mkuu wa Azerbaijan.

Sudan ilivunja uhusiano wa kidiplomasia na Iran mwaka 2016 baada ya uvamizi wa ubalozi wa Saudi Arabia mjini Tehran.

Saudi Arabia na Iran zilirejesha uhusiano wao mwezi Machi chini ya makubaliano yaliyosimamiwa na China, na kuongeza matarajio kwamba Tehran na nchi nyingine za Kiarabu zingeanzisha tena uhusiano wao wa kidiplomasia.

Mkutano kati ya Amirabdollahian na Ali al-Sadiq wa Sudan

Ulifanyika kando ya mkutano wa mawaziri wa nchi zwanachama wa Jumuia ya nchi zisizofungamana na upande wowote uliofanyika Baku.

Chanzo cha habari ya taarifa nii ni Shirika la habari la Reuters