Katibu Mtendaji wa SADC Elias Magosi amesema mkutano wa mawaziri wa afya utaitishwa “kuwezesha utaratibu wa kukabiliana na ugonjwa huo, ambao umeenea katika zaidi ya nchi kumi za Afrika.
Mkutano wa viongozi nchi za jumuiya hiyo ulianza Jumamosi, ambapo Magosi, alitoa “mshikamano na uungaji mkono” kwa wajumbe wa mataifa wanachana walioathiriwa na mpox na kuliomba shirika la Afya Duniani, vituo vya Afrika vya kudhibiti magonjwa na washirika kukabiliana na ugonjwa huo
Wiki hii WHO ilitangaza mlipuko wa mpox Afrika kuwa dharura ya afya duniani.
Katika kanda ya SADC ikiwemo Congo, ambayo ina zaidi ya asilimia 90 ya visa vya mpox.
Wanasayansi pia wametambua aina mpya ya mpox huko Congo ambayo inaweza kuwa na uwezo wa kuambukiza zaidi
WHO imekuwa na wasiwasi wa kusambaa zaidi katika mipaka ya kimataifa , na Sweden imeripoti kisa chake cha kwanza cha kirusi kipya cha mpox.