Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 12, 2024 Local time: 21:01

WHO imetangaza Mpox kuwa ugonjwa hatari kwa afya ya umma duniani


Mkurugenzi mkuu wa WHO
Mkurugenzi mkuu wa WHO

Shirika la afya duniani WHO lilitangaza katika mkutano wake Jumatano kuwa ugonjwa wa Mpox ni dharura ya kimataifa ya afya ya umma.

Mkutano huo ulifanyika siku moja baada ya kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa ya kuambukiza barani Afrika( CDC) kuutaja ugonjwa huo kama dharura ya afya ya umma barani humo, huku visa vikiwa vimeongezeka kwa asilimia 160 tangu mwaka jana na vifo kuongezeka kwa asilimia 19, ukiwa umetangazwa kwa mara ya kwanza kama hatari kwa afya ya umma barani Afrika.

Tangazo hilo la WHO linafanya iwe rahisi kuharakisha mchakato wa kupata na kutekeleza ufadhili, kuchukuliwa kwa hatua za kimataifa za afya ya umma na kuwepo juhudi za pamoja kudhibiti ugonjwa huo. Linasaidia pia kwa kuharakisha utafiti.

Aina mbili kuu za virusi vya mpox zinajulikana kama Clade I na Clade II. Kirusi kisichokuwa na ukali, Clade II B, kilisababisha mlipuko wa kimataifa mwaka 2022, ambao WHO iliutangaza kama dharura ya afya ya umma.

Mkurugenzi wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus alizungumzia mlipuko huo mpya katika hotuba yake ya kufungua mkutano Jumatano, akisema

“Hatukabiliani tu na mlipuko mmoja aina ya Clade one, tunakabiliana na milipuko kadhaa ya aina tofauti za clade katika nchi nyingi na njia tofauti za maambukizi na viwango tofauti vya hatari”, akiongeza kuwa “jibu sahihi na madhubuti linahitajika kushughulikia ugonjwa huo.

Forum

XS
SM
MD
LG