Marekani yasema iko tayari kukutana na Iran

Brian Hook

Marekani imeeleza nia yake ya kujadili mkataba na Iran ambao utahusisha makombora ya ballistika na programu ya nyuklia ya Iran, mwakilishi maalum wa Marekani Iran amesema Jumatano, kabla ya mikutano ya Umoja wa Mataifa itakayo fanyika New York wiki ijayo kuanza.

“Mkataba huo mpya ambao tunatarajia tutaweza kusaini na Iran, na sio makubaliano binafsi, kati ya serikali mbili, kama ilivyo kuwa ule wa kwanza, tunataka mkataba,” mwakilishi Brian Hook amewaambia umati uliyo kuwa umekusanyika katika Taasisi ya utafiti ya Hudson.

Lakini Hook amesema viongozi wa Iran wamekuwa hawana nia ya mazungumzo pamoja na tamko la Rais Donald Trump na Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo mwaka huu likieleza nia yao ya kuwa tayari kukutana nao.

Trump alitangaza mwezi May kuwa anaiondoa Marekani kutoka katika makubaliano yaliyo kuwa yamefikiwa na utawala wa Obama na kusainiwa na Iran na mataifa makubwa sita.

Makubaliano hayo ya 2015 yalikuwa yakiutendaji ambayo yalikuwa hayajapitishwa na Baraza la Seneti ya Marekani. Mkataba utahitaji kupitishwa na Baraza la Seneti.

Wanao pinga mkataba wa Nyuklia wamekuwa wakidai kuwa kushindwa kwa Obama kupata ridhaa hiyo juu ya makubaliano yake na Iran uliwezesha Trump kufutilia mbali makubaliano hayo mwezi Mei.