Haikubainika mara moja ni lini Ukraine inaweza kupokea ndege hizo, ambazo imekuwa ikitafuta kwa muda mrefu ili kukabiliana na Russia, yenye uwezo mkubwa wa ndege za kivita.
Katika ujumbe kwenye mtandao wa X, ambao awali ulilojulikana kama Twitter, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi Wopke Hoe-k-stra alisema: "Tunakaribisha uamuzi wa Washington wa kuandaa njia ya kutuma ndege za kivita za F-16 nchini Ukraine."
Ni lazima Marekani iidhinishe utoaji wa F-16 kwa sababu ndege hizo zinatengenezwa nchini humo.
"Licha ya habari hizo, haikufahamika mara moja, itachukua muda gani kabla ya Ukraine kuzipokea," shieika la habari la AP liliripoti.
Marubani lazima wapate mafunzo ya kina kabla ya Ukraine kupokea ndege hizo.
Mapema siku ya Ijumaa, Ukraine ilijaribu kufanya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani mjini Moscow, lakini vikosi Russia viliidungua ndege hiyo.
Vifusi vya ndege hiyo vilianguka kwenye Kituo cha Maonyesho cha Moscow, eneo kubwa, lililoko chini ya maili 4 kutoka Kremlin.