Ripoti hizo, zikinukuu data kutoka hifadhi ya data ya mauaji ya watu iliyokusanywa na USA Today, Associated Press na Chuo Kikuu cha North Eastern, zikisema kwamba visa viwili vya ufyatuaji risasi huko Texas na Washington katika chini ya dakika 90 Jumapili alasiri viliiweka nchi kwenye "hatua mbaya" kutokana na idadi ya mauaji ya watu wengi kwa mwaka.
Visa hivyo viwili vimechangia idadi ya waathiriwa kutoka kwa visa vya mauaji ya halaiki ya mwaka huu hadi 197, pasi na kujumuisha wahalifu, rekodi nyingine tangu 2006, ripoti hiyo ilisema, ikiongeza kuwa watu wengine 91 walijeruhiwa katika ufyatuaji risasi.
Wataalamu wa masuala ya uhalifu Marekani walisema kuwa ongezeko la visa vya ufyatuaji risasi katika miaka iliyopita viliongeza wasiwasi kuhusu upatikanaji rahisi wa bunduki nchini humu.