Mkutano huo ambao umeandaliwa na Ujerumani na Umoja wa Mataifa, UN, unawashirikisha maafisa kutoka nchi 17 na ulidhihirisha kuunga mkono uchaguzi wa kitaifa nchini Libya ambao umepangwa kufanyika mwezi Disemba 2021.
Afisa wa ngazi ya juu kwenye Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Jumatano aliwambia waandishi wa habari kwamba uchaguzi ni wa muhimu sana sio tu kwa kuhalalisha serikali ya Libya ya muda mrefu, lakini pia kufikia lengo la kuomba wapiganaji wote wa kigeni kuondoka Libya.
Taarifa rasmi ya wanaoshiriki mkutano huo imesema majeshi yote ya kigeni na mamluki wanatakiwa kuondoka nchini Libya bila kuchelewa, lakini Uturuki ilijizuia kutoa msimamo wake.
Chanzo cha Habari : VOA News