Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 14:23

Italia yaisihi Libya kuhakikisha usitishaji vita unadumishwa na kuzingatiwa


Waziri mkuu wa Italia Mario Draghi akihutubia bunge la Italia huko Roma, Feb. 18, 2021.
Waziri mkuu wa Italia Mario Draghi akihutubia bunge la Italia huko Roma, Feb. 18, 2021.

Waziri Mkuu wa Italia Mario Draghi Jumanne aliisihi serikali ya Libya kuhakikisha kuwa usitishaji vita nchini humo unadumishwa na kuzingatiwa kwa kiasi kikubwa.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters katika mazungumzo na waandishi wa habari pamoja na Waziri Mkuu wa mpito wa Libya Abdulhamid Dbeibeh, Draghi alisema viongozi hao wawili walizungumza juu ya uhamiaji na ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili na uhusiano mkubwa wa kihistoria.

"Ili Libya iweze kuendelea kwa ujasiri na uamuzi ni sharti kwamba usitishaji wa mapigano lazima uendelee na uzingatiwe kabisa," Draghi alisema baada ya safari yake ya kwanza ya nje ya nchi tangu aingie madarakani mwezi Februari.

Serikali mpya ya umoja inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ya Dbeibeh ilichukua madaraka mwezi uliopita ikiwa na jukumu la kuboresha huduma na kujiandaa kwa uchaguzi wa kitaifa mwezi Desemba.

Libya imegawanyika kutokana na ghasia na vurugu kwa muongo mmoja tangu mapinduzi yalioungwa mkono na NATO mwaka 2011 dhidi ya Muammar Gaddafi na kugawanyika kati ya vikundi vya magharibi na mashariki mwaka 2014.

XS
SM
MD
LG