Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 13:27

Waziri mkuu wa Libya kuanza ziara ya Uturuki


Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan

Waziri mkuu wa Libya, Abdulhamid Dbeibeh, na ujumbe wa mawaziri atafanya ziara ya kwanza ya Uturuki, Jumatatu kwa mujibu wa ofisi ya rais wa Uturuki.

Serekali mpya ya umoja wa kitaifa iliapishwa Machi 15 kutoka pande mbili za utawala zilizokuwa na uhasama ambazo zilikuwa upande wa mashariki na magharibi mwa nchi na kuamua kumaliza tofauti zao kwa njia ya amani baada ya muongo mmoja wa ghasia.

Uturuki ilikuwa inaunga mkono serekali ya Tripoli ya GNA dhidi ya serekali ya mashariki ya LNA iliyokuwa ikiungwa mkono na Russia, Misri, Falme za kiarabu na Ufaransa.

Ofisi ya rais wa Uturuki imeeleza kwamba Dbeibeh atafanya ziara ya siku mbili baada ya kupokea mualiko wa rais wa Uturuki, Tayyip Erdogan na kueleza kwamba watafanya mkutano wa ngazi ya juu wa mikakati ya kuboresha ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili.

XS
SM
MD
LG