Marekani kutoa msaada mpya wa dola milioni 100 kwa visiwa vya Caribbean

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris

Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris atatangaza zaidi ya dola milioni 100 za msaada mpya kwa visiwa vya Caribbean.

Kamala anafanya ziara huko Bahamas hii leo Alhamisi. Marekani wakati huo wa ziara yake na itafunguwa ofisi mbili za ubalozi wa Marekani nchini humo.

Zaidi ya dola milioni 50 zitatumika kwa msaada wa kibinadamu kwa Haiti, afisa mkuu wa utawala wa Marekani alisema.

Harris, afisa wa ngazi ya juu zaidi wa Marekani kutembelea Bahamas tangu uhuru wake mwaka 1973, na Waziri Mkuu wa Bahamas Philip Davis watakuwa wenyeji wa viongozi wa Caribbean huko Nassau.