Wakizungumza na shirika la habari la AFP, maafisa hao walisema uungwaji mkono wa nchi za Magharibi pia ni muhimu katika kukomesha kundi la mamluki la Wagner la Russia ambalo limefanya mashambulizi makubwa katika nchi zinazokumbwa na ghasia za Sahel, ikiwa ni pamoja na kushirikiana na serekali ya kijeshi ya Mali.
Makamu wa Rais Kamala Harris, alipoitembelea Ghana mwezi uliopita ikiwa sehemu ya juhudi zinazoongezeka za Marekani barani Afrika, aliahidi dola milioni 100 kwa miaka 10 ili kuimarisha uthabiti katika pwani ya Afrika Magharibi.
Maafisa wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani pia wanaangalia ufadhili wa ziada ikiwa ni pamoja na kutoka kwa bajeti ya kukabiliana na ugaidi.