Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:48

Unaposhambulia Haki za Wanawake Marekani unaishambulia Marekani; Harris


Makamu Rais wa Marekani, Kamala Harris akizungumza kwenye mikutano inayoelezea haki za utoaji mimba huko Los Angeles, Apr. 15, 2023.
Makamu Rais wa Marekani, Kamala Harris akizungumza kwenye mikutano inayoelezea haki za utoaji mimba huko Los Angeles, Apr. 15, 2023.

Mahakama ya Juu Marekani ilisitisha kwa muda sheria ya serikali kuu ya matumizi ya dawa za vidonge za utoaji mimba baada ya uamuzi wa mahakama ndogo kutaka kuzuia matumizi ya vidonge hivyo ambavyo wanawake wamekuwa wakitumia kwa miaka mingi

Makamu Rais wa Marekani Kamala Harris alifika kwenye maandamano ya haki za utoaji mimba mjini Los Angeles nchini Marekani siku ya Jumamosi katika moja ya mikutano kadhaa ya aina hiyo iliyofanyika kote nchini humo kufuatia maamuzi ya hivi karibuni ya mahakama yanayozuia fursa ya utoaji mimba.

Unaposhambulia haki za wanawake nchini Marekani, unaishambulia Marekani, Harris aliuambia umati wa watu. Siku ya Ijumaa, Mahakama ya Juu Marekani ilisitisha kwa muda sheria ya serikali kuu ya matumizi ya dawa za vidonge za utoaji mimba baada ya uamuzi wa mahakama ndogo kutaka kuzuia matumizi ya vidonge hivyo ambavyo wanawake wamekuwa wakitumia kwa miaka mingi.

Majaji wanatakiwa kuzingatia tu ni sehemu gani za uamuzi wa Aprili 7 uliotolewa na Jaji wa Wilaya katika jimbo la Texas, Matthew Kacsmaryk kutokana na ilivyobadilishwa na uamuzi wa rufaa Jumatano na kama inawezekana kutumika wakati kesi hiyo ikiendelea.

Agizo hilo linaisha muda wake Jumatano jioni.

XS
SM
MD
LG