Katika kura hiyo ya Jumatano, wabunge 314 walipitisha mswada huo dhidi ya 117, walioupinga. Baada ya hapo, mswada huo sasa unaelekea kwenye baraza la Seneti ambapo utapigiwa kura kufikia mwishoni mwa wiki.
Endapo utapitishwa na seneti, baraza ambalo linadhibitiwa na Wademokrat kwa wingi wa wajumbe, basi Rais Biden atautia saini na kuwa sheria.
Hatua hiyo inasimamisha kiwango cha sasa cha deni la serikali la $31.4 trilioni.
Wabunge wa chama cha RepubliKan wenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia, wamekosoa makubaliano yaliyofikiwa na Rais Mdemokrat Joe Biden na Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mrepublikan Kevin McCarthy kwa kutopunguza vya kutosha, matumizi ya serikali ya siku za usoni, huku baadhi ya Wanademokrat wakitofautiana kuhusu suala hilo.